Full-Width Version (true/false)


Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery ameanza kwa style hiiKocha mpya wa Arsenal, Unai Emery ameanza usajili na beki, Stephan Lichtsteiner mwenye umri wa miaka 34.

Usajili huo umekuwa wa kwanza tangu Emery atue Arsenal akitokea PSG ya Ufaransa kuja kuchukua nafasi ya Arsene Wenger aliyeitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 21.

Emery anaamini beki huyo kutoka Juventus ya Italia atakuwa kiongozi wa wenzake katika kazi ya ulinzi.

Lichtsteiner amejiunga na Arsenal akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na kibibi kizee cha Torino huko Italia.

No comments

Powered by Blogger.