Full-Width Version (true/false)


Kocha Simba afunguka Marcel Kaheza kucheza dakia 20 tu "Nilimtoa Kaheza Kwavile Hakufuata Maelekezo Yangu"DAKIKA 20 alizocheza mshambuliaji mpya wa Simba, Marcel Kaheza katika mchezo wa jana dhidi ya k.sharks kwenye mchezo wa sportpesa super cup zimezua sintofahamu kwa mashabiki wa soka ,wengi wakijiuliza kwanini kocha mkuu wa  Wekundu hao, Pierre Lechantre aliamua kumtoa haraka hivyo.


Kaheza ambaye amesajiliwa hivi karibuni kutoka Majimaji ya mjini Songea aliingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mohamed Ibrahim ambaye hakuwa katika kiwango bora lakini alitolewa dakika ya 65 akiwa amedumu uwanjani kwa dakika 20 pekee huku Shiza Kichuya akichukua nafasi yake.

Baada ya pambano hilo ambalo lilimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa penati 3-2 Lechantre aliwaambia wanahabari kuwa Kaheza hakufanya kile alichomwagiza kwenda kufanya na alikuwa na hofu ndio sababu aliamua kumtoa.

“Nilimwambia aingie akapambane lakini yeye hakufanya hivyo, ndio sababu niliamua kumtoa kwavile simpi nafasi mchezaji kama zawadi,” alisema.
Nyota mwingine aliyesajiliwa hivi karibuni kutokea Prisons ya Mbeya, Mohamed Rashid alianza pambano hilo ingawa alimpisha Moses Kitandu dakika za mwishoni. Hata hivyo alionekana kutoelewana vema na wenzake kutokana na ugeni kikosini hapo. 
credit:boiplus

No comments

Powered by Blogger.