Full-Width Version (true/false)


Kumbe Hamisa na Diamond walishaonywa mapema

 

Drama bado haziishi kwa upande wa Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto.
Kwa sasa meneja wa Diamond, Babu Tale amesema kabla ya Hamisa kuzaa na Diamond alishawaonya kwani wakati huo Diamond alikuwa katika mahusiano na Zari.

“Kabla Hamisa hajapata ujauzito, tulikuwa tuna-shoot video ya Salome nikamwambia Zari sio adui yako, kama una mapenzi na Diamond mpende ila kama unataka kumkomesha, kamkomeshe Lulu, ila kama unataka kufanya hivyo haipendezi,” amesema. 

“Nikamwambia pia Diamond kama unafanya ujana, inatakiwa pia uangalie ujana wako yule demu (Zari) amekuja huko from nowhere amekuzalia mtoto pia,” Tale ameiambia Wasafi TV.

Moja ya sababu alizoeleza Zari kuwa zilichangia kuachana na Diamond Platnumz ni kitendo cha kuzaa na Hamisa Mobetto. Babu Tale kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kuhakikisha Diamond na Zari wanamaliza tofauti zao.

No comments

Powered by Blogger.