Full-Width Version (true/false)


Kumbe Mo Rashid anawajua vizuri Okwi na Bocco!

 

Mshambuliaji mpya wa Simba, Mohammed Rashid 'Mo Rashid' amesema, ataanza kuonyesha makali yake ndani ya kikosi hicho katika mashindano ya SportPesa yanayoendelea nchini Kenya na kwamba Wekundu hao hawatajutia usajili wake. 

Mo Rashid aliyesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Tanzania Prisons, ameongea hayo kwa sababu hana wasiwasi na ushindani wa namba ndani ya Simba. 

Amesema, anawajua vizuri washambuliaji wa Simba kama John Bocco 'Adebayor', Emmanuel Okwi na Marsel Kahesa na anakiamini kiwango chake. "Nimekuja Simba natambua kuna washambuliaji wenye uwezo ambao lakini hata mimi ninao ndiyo maana wamenisajili na nitatumia mashindano haya kucheza kwa bidii ili nilishawishi benchi la ufundi kunipa nafasi ya kucheza zaid," amesema Mo Rashid. 

"Nimekiangalia kikosi cha Simba msimu huu haswa katika safu ya ushambuliaji ambayo mimi ndiyo nacheza, kuna Bocco ambaye anauwezo wa kufunga lakini hana kasi katika kucheza kwake, mimi naweza kumzidi kwa sababu ninafunga na kasi ninayo. 

"Okwi nafahamu ni roho ya timu lakini mara nyingi huwa na eneo ambalo ndiyo anacheza muda wote, mimi ninauwezo wa kupambana na kuzunguka eneo lote la mbele. Marcel Kaheza

No comments

Powered by Blogger.