Full-Width Version (true/false)


KWA MARA YA KWANZA, KAHEZA ATUPIA UZI WA SIMBA BAADA YA KUREJEA NA KUANZA KUJIFUA

Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Marcel Kaheza kwa mara ya kwanza ameanza mazoezi na timu yake hiyo.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameanza mazoezi mjini hapa.

Kaheza amejiunga na Simba akitokea Majimaji FC ya Songea ambayo alijiunga nayo akitokea Simba akiwa mmoja wa wachezaji makinda.

Simba wako hapa kwa ajili ya michuano ya SportPesa Super Cup na wataanza kazi Jumatatu kwa kuwavaa Sharks.

Simba wamewasili hapa jana wakiwa ndiyo timu ya kwanza ya Tanzania kutua Kenya kwa ajili ya michuano hiyo.

Mwaka jana ilifanyika Tanzania na Gor Mahia wakaibuka mabingwa huku timu za Kenya zikikutana katika fainali.

No comments

Powered by Blogger.