Full-Width Version (true/false)


Kwa mkwanja huu Zidane hakuwa na budi kuiacha MadridKocha ambaye ameondoka ndani ya Real Madrid, Zinedine Zidane maarufu kwa jina la Zizzou amesaini mkataba mnono wa kuifundisha timu ya taifa ya Qatar. 

Mkataba huo wa miaka minne una thamani ya Pauni Milioni 176 (Sh Bilioni za Kitanzania 531) kwa miaka minne mpaka 2022.

Mkataba huo utamuingizia Mfaransa huyo kiasi cha Pauni Milioni 50 kwa mwaka (zaidi ya Tsh Bilioni 142). Hii ina maana kwa siku, Zidane atakuwa anaingiza zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 362.

Alipokuwa Real Madrid, Zidane alikuwa analipwa mshahara wa Pauni Milioni 4.8 kwa mwaka. Hii inamaanisha mshahara wa sasa wa Zidane ni zaidi ya mara 10 ya ule aliokuwa analipwa Real Madrid.

Dau hilo linamfanya Zidane kuwa kocha wa soka anayelipwa fedha nyingi kuliko kocha yeyote duniani na kumpiku Marcelo Lippi.

Ifuatayo ni orodha ya makocha Watano wanaolipwa pesa nyingi zaidi;

1.Zinedine Zidane (Timu ya Taifa ya Qatar), pauni Milioni 50 kwa mwaka

 2.Marcelo Lippi (Timu ya Taifa ya China), pauni milioni 18 kwa mwaka

3.Pep Guardiola (Manchester City, Uingereza) pauni milioni 15.3

4.Jose Mourinho (Manchester United, Uingereza), pauni million 15

5.Fabio Capello (Jiangsu Suning, China) pauni milioni 8.98

No comments

Powered by Blogger.