Full-Width Version (true/false)


Lechantre atinga tuzo za MO

 

Kocha wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre saa 12:35 jioni akifika katika ukumbi wa Kilimanjaro hoteli katika hafla ya ugawaji tuzo. Jioni hii Simba uongozi wa Simba uligawa tuzo mbalimbali katika hapa Kilimanjaro na wageni mbalimbali waliudhuria. 

Tuzo hizo zinazotambulika kwa jina la MO Simba Awards ambazo kwa mara ya kwanza zinatoka katika klabu hiyo ambayo imechukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu. Lechantre alifika hapa akiwa na kocha wa viungo Mohammed Habib ambao waliketi katika meza moja.

 Lechantre aliugomea uongozi wa Simba katika mashindano ya Sport Pesa nchini Kenya na kuondoka na kukiacha kikosi hiko kikiwa bado kinaendelea na mashindano. Licha ya Lechantre kuondoka lakini mapema leo jioni hii alijitokeza katika ukumbi huu wa Kilimanjaro

No comments

Powered by Blogger.