Full-Width Version (true/false)


Lechantre hana uhakika Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre amesema, anashindwa kuendelea kupanga mipango mingi ndani ya Simba kwani mpaka sasa hafahamu hatma yake na huenda asiendelee tena kuinoa timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam. 

Lechantre amesema mpaka sasa hajafikia makubaliano yoyote ya mkataba mpya na Simba, lakini anamsikilizia mfadhali wa timu hiyo, Mohammed Dewji juu ya hatma yake hiyo. “Nimegundua hapa watu wana matarajio makubwa sana. 

 Niliposhinda mechi nyingi walikuwa kimya, tulipofungwa na kutoa sare watu wameumia sana. Nahitaji kupewa muda zaidi ili nitengeneze timu mpya,"amesema Lechantre. “Mohammed Dewji ana programu nzuri hapa, inahitaji muda. 

Ni lazima tukubaliane kwamba kutengeneza timu ya kushinda taji la Afrika inahitajika muda zaidi, nitazungumza naye ili kuona tunafanya nini. 

“Mpaka sasa sijafahamu hatma yangu, nashindwa kupangilia vituvingi hivyo hata hao wachezaji wapya siwezi kusema nitawatumia vipi,” amesisitiza Mfaransa huyo aliyeomba kazi tena timu ya Taifa ya Cameroon

No comments

Powered by Blogger.