Full-Width Version (true/false)


Lechantre kuhudhuria tuzo za Mo Simba Awards
Kocha Mfaransa Pierre Lechantre anatarajiwa kuwa miongoni mwa watu watakaohudhuria hafla ya ugawajwi wa tuzo za Mo Simba Awards katika Ukumbi wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam jioni hii.

Taarifa zinaeleza Lechantre atahudhuria hafla hiyo ambayo itatoa tuzo mbalimbali zilizoanzishwa na mwekezaji wa klabu Mohammed Dewji 'Mo'.

Tuzo hizo zinatolewa kwa baadhi ya viongozi na wachezaji waliofanikisha klabu hiyo kufikia hapo ilipo kwa sasa ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu uliomalizika (2017/18).

Mbali na wachezaji pamoja na mashabiki, tuzo hizo zitatolewa kwa shabiki bora wa mwaka pamoja na tawi bora lililotoa mchango wake mzuri katika kikosi cha Simba kwa msimu wa 201718.

Lechantre ambaye anatajwa kuondoka Simba na nafasi yake aikaimu Mrundi, Masoud Djuma, atakutana na bosi wake Dewji ambaye ndiye mhusika mkuu wa tuzo hizo.

Mfaransa huyo alisusia kuingoa Simba kwenye mashindano ya SportPesa Super Cuo huko Nakuru, Kenya kwa madai ya kutaka apewe mkataba mpya baada ya ule wa miezi sita kuelekea ukiongoni mwezi huu.

No comments

Powered by Blogger.