Full-Width Version (true/false)


Ligi kuu ya England yafanyiwa mabadilikoChama cha soka nchini England (FA) kimetangaza mabadiliko kwenye ligi kuu ya EPL ambapo sasa itakuwa na mapumziko ya wiki mbili ndani ya mwezi Februari ambayo ni majira ya baridi nchini humo. 

Kwa mujibu wa taarifa ya FA iliyotolewa mchana huu imeeleza kuwa vilabu vya Ligi Kuu vitakuwa na mapumziko majira ya baridi mwezi Februari kuanzia msimu wa 2019/20.

Mapumziko hayo yatafanyika kwa mtindo wa mechi tano kupigwa kwenye wikiendi ya kwanza ya mwezi Februari na zingine tano kupigwa wikiendi ya pili. Timu zote 20 zitapumzika kwa wiki mbili za mwisho ndani ya mwezi Februari.

Kwa upande mwingine FA wameeleza kuwa michuano ya Kombe la FA nayo itabadilishwa kutoka kuchezwa wikiendi hadi katikati ya wiki kwa mechi za mwezi Februari ili kutoa fursa kwa mapumziko ya EPL kutekelezwa.

Awali vilabu vililalamika wachezaji kuchoka kutokana na kukosa mapumziko kwenye majira ya baridi huku ligi zingine zikitoa mapumziko kwa timu kwenye wiki mbili za mwisho ndani ya mwezi Desemba.

No comments

Powered by Blogger.