Full-Width Version (true/false)


“Ligi kuu yetu haina ubora”- Julio
Kocha wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo maarufu kama Julio, amesema ligi ya Tanzania Bara haina ubora unaotakiwa wa kufanya timu zinazoshiriki ligi hiyo kuweza kutoa ushindani dhidi ya timu za mataifa mengine katika mashindano mbalimbali. 


Kocha Julio amesema hayo leo Juni 8, 2018 akiongea na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa hisani kusadia uchangiaji wa fedha milioni 50 katika sekta ya elimu na kuongeza kuwa kama Taifa ni bora kuangalia ni wapi sekta ya michezo inakwama kuanzia ngazi ya vilabu mpaka Taifa.


“Niseme kwamba tunachangamoto nyingi sana katika mpira wetu wa Tanzania bahati mbaya, Julio ninapokuwa mkweli watu huwa wananichukia, mfano Simba, klabu bingwa wa Tanzania lakini angalia Kenya tunacheza na timu inaitwa Kariobangi tumetoa sare, hii ni kuonesha kwamba ligi ya kwetu haina ubora sana” amesema Julio.

Julio ameongeza kuwa viongozi wa soka nchini wamekua mabingwa wakuongea mipango mingi mizuri lakini hakuna utekelezaji na hupelekea kudumaa kwa sekta ya michezo nchini na kuongeza kuwa ni lazima kutafuta njia muafaka ya kupita ili kufikia mafanikio ya soka.

Kesho Juni 9, 2018 utafanyika mchezo maalumu wa hisani wa kusaidia sekta ya elimu nchini ambapo utazikutanisha timu ya mashabiki wa mbwana Samatta na wapenzi wa msanii wa muziki nchini Alikiba na mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.