Full-Width Version (true/false)


Ligi tano bora za soka barani Ulaya zavunja rekodi
Ligi Kubwa tano za soka Barani Ulaya zimevunja rekodi ya mapato kwa msimu wa mwaka 2016/17 kwa kuingiza Euro bilioni 14.7 likiwa ni ongezeko la asilimia 9 kwa mwaka.

aarifa iliyotolewa na kampuni ya Delloitte imesema, soko la soka Barani Ulaya kwa sasa lina thamani ya Euro bilioni 25.5, huku Ligi Kuu ya nchini Uingereza, maarufu kama EPL ikiongoza kwa mapato ya Paundi bilioni 4.5.

Imeelezwa kuwa, kwa ukubwa wa mapato EPL ina asilimia 86 zaidi ya mpinzani wake wa karibu ambayo ni Ligi Kuu ya Hispania La Liga.


Deloitte imesema kwa pamoja vilabu vya 92 vinavyoshiriki katika Ligi hizo vimeingiza mapato ya Paundi bilioni 5.5, ambapo mapato ya Ligi Kuu ya Uingereza yaliongezeka na kufikia Paundi bilioni 4.5 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 25, ambapo katika mwaka wa kwanza wa haki za matangazo ukishuhudia kila klabu ya EPL ikilipwa kati ya Paundi milioni 95 mpaka Paundi 150.

Wakati huo huo taarifa zinasema, Ligi Kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga ikitajwa kuwa Ligi ambayo ilikuwa na uwiano mzuri wa mashabiki kuhudhuriwa viwanja kwa wastani wa watazamaji elfu 40 kwa kila mechi.

Nayo mapato ya Ligi Kuu ya Nchini Italia ya Serie A yaliongezeka kwa asilimia 8 na kufikia zaidi ya Euro bilioni 2 kwa mara ya kwanza huku asilimia kubwa ya ongezeko hilo likitokana na vyanzo vya kibiashara.

No comments

Powered by Blogger.