Full-Width Version (true/false)


Magari yaliyotumika miaka 15 yapigwa marufuku
Magari yaliotumika kwa zaidi ya miaka 15 hayatoruhusiwa nchini Uganda kuanzia Septemba mwaka huu kufuatia kuidhinishwa kwa marekebisho ya mswada wa trafiki na usalama barabarani mwaka 2018.
 
Watu wengi hununua magari makuu kuu kwasababu ya gharama zake kuwa chini lakini serikali inataka kusitisha magari hayo kuingia nchini humo ikieleza kuwa sio salama kwa matumizi na huchafua mazingira.

Sheria hiyo mpya imenuiwa kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na kusaidia kupunguza ajali barabarani ambazo kwa kiwango kikubwa zimetajwa kutokana na magari ya zamani.

Utafiti wa kimazingira hivi karibuni umebaini kuwa Kampala ni mojawapo ya miji inayoshuhudiwa uchafuzi mkubwa wa mazingira Afrika.

No comments

Powered by Blogger.