Full-Width Version (true/false)


Majambazi wanne wauawa kwa kupigwa risasi Shinyanga.

 
Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limewaua kwa kuwapiga risasi watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu wakituhumiwa kufanya uhalifu kwa kutumia silaha katika mikoa mbalimbali ya kanda ya ziwa na kufanikiwa kukamata bunduki mbili moja ikiwa ni yakivita aina ya AK 47 na short gun moja iliyokatwa mtutu,  bastola 2, bomu moja la kutupa kwa mkono na risasi 45 zikiwa katika magazine mbili tofauti. 

Kamanda wa polisi mkoa wa SHINYANGA ACP Simon Haule amesema watu hao wamepoteza maisha wakiwa njiani kupelekwa katika hospitali ya Kahama mji kufuatia majeraha ya risasi waliyoyapata kwa kupigwa risasi na polisi wakati wakijaribu kutoroka baada ya kuonesha silaha hizo na eneo wanalolitumia kuzicha baada ya kufanya uhalifu. 

Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi cha mkoa wa Shinyanga Afande Amedeus Tesha amesema oparesheni hiyo imefanyika kwa muda wa siku tano katika mikoa ya Tabora,Kigoma na Shinyanga hususani wilayani Kahama ambapo mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Masalamali Paulo alikamatwa mkoani Kigoma na kuwataja wenzake watatu ambapo amewataka watu wanaojihusisha na ujambazi kujisalimisha na silaha zao kabla ya kukamatwa. 

Baadhi ya wakazi wanaoishi katika eneo la Makaburi ya Kitwana nje kidogo ya mji wa Kahama lenye vichaka vinavyotajwa kutumiwa na wahalifu wamelipongeza Jeshi la polisi kufanya oparesheni hiyo na kudai kuwa watu wengi wasiojulikana wanakotoka wamekuwa wakionekana wakika katika eneo hilo mchana na usiku na kuondoka bila kujulikana wanachokifanya

No comments

Powered by Blogger.