Majambazi yampora Sh39 milioni mfanyabiashara wa ng’ombe

Majambazi hayo yakiwa wamefunika sura zao na vitambaa vyeusi huku
wakiwa na silaha zinazodaiwa kuwa SMG, walimvamia mfanyabiashara
huyo nyumbani kwake mtaa wa Mwayunge, kata ya Igunga Mjini
wilayani Igunga Juni 2.
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Wilbrod Mutafungwa alisema
polisi wanaendelea kuyasaka majambazi hayo na kuwataka wananchi
kutoa ushirikiano watakapopata taarifa yalipo.
Akizungumzia tukio hilo, Ramadhan alisema lilitokea Jumamosi saa
1:00 jioni wakati akifuturu na familia nyumbani kwake.
Ramadhan alisema majambazi hayo baada ya kufika nyumbani
yaligawanyika sehemu tatu; moja lilibaki getini, jingine lilimteka mmoja
wa mtoto wake ili alionyeshe sehemu ya kuzimia taa huku jingine
likimuamuru atoe fedha
kwenye gari yake alipokuwa amezihifadhi.
No comments