Full-Width Version (true/false)


Majeruhi 13 wa ajali ya basi na treni wapata ahueniMajeruhi kumi na Tatu kati ya thelathini na tano walionusurika kifo katika ajali ya basi lililogonga treni ya mizigo mkoani Kigoma wameruhusiwa kutoka katika hospitali ya Rufaa Maweni walipokuwa wakipatiwa matibabu baada ya afya zao kuimarika.


Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Rufaa Maweni mkoani Kigoma Dk. Osmond Dyegula amesema wametoa ruhusa kwa wagonjwa hao baada ya kujiridhisha na hali zao na kwamba majeruhi wengine 22 wanaendelea na matibabu licha ya mmoja wao kuonekana kuwa na hali mbaya.


Kwa upande wao baadhi ya ndugu wa marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo, wameiomba serikali kuweka alama na vizuizi katika eneo ilipotokea ajali hiyo kutokana na eneo hilo kuwa katikati ya makazi ya watu hivyo kuwa vigumu kumuona mtu au Gari moshi linapotokea.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jonh Magufuli ametuma salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki walio ondokewa na wapendwa wao sambamba na Serikali ya Mkoa kiujumla ambapo amezitaka mamlaka zinazohusika na usalama barabarani kuchukua hatua dhidi ya madereva wasiofuata na kuzingatia sheria za usalama wa barabarani.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samsoni Anga ametoa pole na kuwatakia heli ya matibabu majeruhi waliopo hospitali ya Rufaa Maweni nakuongeza kuwa msiba uliotokea ni msiba wa mkoa na umegusa kila mmoja.


No comments

Powered by Blogger.