Full-Width Version (true/false)


Makamu wa Rais Afurahishwa na miundombinu Hospitali ya Mloganzila aagiza kuongezwa bajeti ya dawa

Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameonyesha kuridhishwa na miundombinu ya utoleaji wa huduma za afya katika hospitali ya taaluma na tiba ya chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi Muhimbili kampasi ya Mloganzila na kumuagiza waziri wa afya kuongeza bajeti ya dawa kwa hospitali hiyo kutoka shilingi milioni 600 za sasa hadi shilingi milioni 900.
Awali Makamu wa Rais alipata fursa ya kutembelea wodi kadhaa na kujionea miundombinu ya utolaiji huduma ya afya ambapo ameahidi kutatua changamoto zinazoikabili hospitali hiyo ambazo ni pamoja na tatizo la umeme wa uhakika, idadi ya watumishi pamoja na ukosefu wa usafiri wa uhakika.
Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu anasema hospitali ya Mloganzira inafanya serikali kuwa na jumla ya hospitali 7 zinazotoa matibabu ya juu ya kibingwa huku mtendaji mkuu wa hospitali hiyo Prof. Said Abood akisema mpka sasa wagonjwa 27000 wamekwisha kupatia matibabu na kwmaba tayari oparesheni 307 zimekwisha kufanyika.
Nje ya hospitali hiyo wagonjwa wakamueleza Makamu wa Rais changamoto ya gharama kubwa matibabu wanazokumbana nazo katika hospitali hiyo.
Akijibu malalamiko hayo mtendaji mkuu wa hospitali hiyo amesema wamekuwa wakitoa misamaha kwa wagonjwa wasioweza kulipia matibabu huku makamo wa rais akiwataka wananchi kuhakikisha wanajiunga na bima ya afya.
Katika ziara hiyo makamU wa rais aliambatana na Naibu Waziri Wizara ya Elimu, mganga mkuu wa hospitali na maafisa mbalimbali wandamizi serikali.

No comments

Powered by Blogger.