Full-Width Version (true/false)


Mama Hamisa apata kigugumizi Diamond kumpa mwanaye ujauzito mwingine

 

Wakati habari za ‘ujauzito mpya’ wa Hamisa Mobetto zikizidi kushika kasi kwenye mitandao ya kijamii, mama yake amegoma kuthibitisha akisema hana muda wa kujibu taarifa za mitandaoni. 

Akizungumza na MCL Digital, Mama Hamisa amesema habari ya ujauzito amezisikia katika mitandao na kwamba kama kweli binti yake ana ujauzito basi hilo ni jambo la kheri. "Unajua mimi sipendi sana kuongea ongea na sio kama siwezi ila najijua mimi mtu wa Musoma huwa nakuwa na hasira za karibu sana, ndio maana mambo mengi yanayotokea mitandaoni huwa nakaa kimya ili kulinda heshima yangu. 

 4/2018 Mama Hamisa apata kigugumizi Diamond kumpa mwanaye ujauzito mwingine - Habari | Mwananchi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Mama-Hamisa-apata-kigugumizi-Diamond-/1597578-4596694-sv9ywaz/index.html 3/9 "Mfano hiyo ishu ya Hamisa kuwa mjamzito mimi nimeisikia mitandaoni na kama kweli mimi sioni tatizo, hilo ni jambo la kheri kwetu," alisema Mama Hamisa. Hamisa anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitatu wa mwanamuziki Diamond ambaye pia ni baba wa mtoto wake wa pili Daylan. Mwanamitindo huyo pia ana mtoto mwingine wa kike aliyezaa na mmiliki wa kituo cha redio na televisheni cha EFM na ETV, Dj Majizzo.

No comments

Powered by Blogger.