Full-Width Version (true/false)


Mama Samia aimwagia pongezi Hospitali ya CCBRTMakamu wa Rais, Samia  Suluhu ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa huduma bora wanazozitoa hususan za wagonjwa wa Fistula kwa wanawake kwa miaka 25 kwa kile alichodai kuwa wamefanikiwa wengi kurudisha heshima na utu wa heshima kwa wanawake wengi nchini.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan katika ziara yake kwenye hospitali ya CCRBT leo jijiji Dar es Salaam baada ya kujionea huduma za afya ya Mama na Mtoto zilivyopiga hatua katika jiji hilo.

Mhe. Samia amesema "Hakuna jambo kubwa Duniani kama kumrudishia mtu utu na heshima kwa wanawake waliokuwa wanatenga na hata pengine kukimbiwa, kweli kazi mnayoifanya ni kazi ya Mungu" .

Aidha Samia amesema kuwa  Huduma za afya ya Mama na Mtoto kwa Mkoa wa Dar es Salaam imefikia asilimia 80 ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita  na kuitaka wizara ya afya kushirikiana na ofisi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kupata takwimu zinazofanana kwenye utoaji wa huduma za afya nchi nzima.

"Licha ya Dar es Salaam kufikia asilimia hii ni ya huduma za mama na mtoto bado tunahitaji mafunzo ya kiutendaji na kitaalam kwa watoa huduma za afya ili kupiga hatua zaidi nchi nzima"  Samia.

No comments

Powered by Blogger.