Full-Width Version (true/false)


Mambo yameanza kunoga Yanga, washusha kifaa kipya kutoka BeninMshambuliaji wa kimataifa kutka Benin, Marcellin Koukpo amewasili jana usiku akitokea nchini kwao na kupokelewa na Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten.

Koukpo ambaye alikuwa kwenye mazungumzo ya muda mrefu na uongozi wa Yanga ametua leo tayari kutia kandarasi na mabingwa hao mara 27 wa ligi kuu nchini.

Koukpo ambaye alikuwa akiichezea Les Buffles FC ya huko Benin inaelezwa tayari ameshamalizana kwa kila kitu na Yanga na atasaini mkataba wa miaka miwili.

Taarifa za ndani zinasema Koukpo atakabidhiwa jezi namba 11 ambayo alikuwa akiichezea Donald Ngoma baada ya kuondoka kutimkia Azam FC.

No comments

Powered by Blogger.