Full-Width Version (true/false)


Manara, Kerr wawa kivutio michuano ya sportpesa

  

AFISA Habari wa Simba, Haji Manara na kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr wamekuwa kivutio kikubwa mjini hapa wakati michuano ya SportPesa Super Cup ikiendelea kuwasha moto. 

Manara aliwasili mjini hapa jana Jumapili na kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Yanga waliotua mjini hapa ambao waliomba kupiga naye picha ya kumbukumbu kwa timu yao kudhalilishwa na Kakamega Homeboys. 

Kerr amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Gor Mahia na baada ya timu yake kuichapa JKU ya Zanzibar mabao 3-0 hiyo juzi, walinzi wa Uwanja wa Afraha walilazimika kutumia nguvu ya ziada kumtoa uwanjani kutokana na mashabiki wengi kumsonga wakitaka kupiga naye picha. 

Manara alisema; "Yanga wametukimbia, walifahamu wazi kuwa wakishinda wanaweza kukutana nasi lakini wamekimbia. Simba itafuta aibu ya Tanzania."

No comments

Powered by Blogger.