Full-Width Version (true/false)


Manuel Pellegrini alishukuru Jeshi la Polisi baada ya kunusurika mikononi mwa vibaka


 
Meneja wa klabu ya West Ham United, Manuel Pellegrini amelishukuru jeshi la polisi la nchini Chile baada ya kunusurika mikononi mwa vibaka wenye silaha kali wakati walipotaka kupora.


Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter, Pellegrini amewashukuru polisi wa nchi hiyo kwakufika muda muafaka eneo la tukio mara baada ya vibaka hao waliyokuwa na silaha za moto walipo wavamia wakati kocha huyo akiwa na mkewe, Carola Pucci kwenye  ‘restaurant’ huko Santiago suburb Vitacura usiku wa Jumamosi.

Ujumbe huo unasema kuwa ”Pongezi kwa 

Hata hivyo hakuna aliyeumia kwenye tukio hilo licha ya kuripotiwa kuwa mke wa Pellegrini, Carola Pucci ameibiwa mkoba wake ‘handbag’ kupitia wezi hao huku polisi wakifyatua risasi wakati wakiwafukuza hali iliyopelekea kupata ajali kwa gari lao.

Kocha huyo raia wa Chile amewahi kuiongoza klabu ya Manchester City kwa mafanikio makubwa kwenye ligi kuu nchini Uingereza na kabla ya kutua West Ham hivi karibuni alikuwa akiifundisha timu ya Hebei China Fortune ya China.

No comments

Powered by Blogger.