Full-Width Version (true/false)


Manula azua hofu Simba

 


Shujaa wa Simba, Aishi Manula amezua hofu  baada ya kupata majeraha yaliyomfanya akose mazoezi ya leo Jumanne asubuhi huko Nakuru nchini kenya ambako mashindano ya sportpesa yanaendelea.. 

Manula aliumia katika dakika ya 76 ya pambano la robo fainali la michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kugongana na beki Paul Bukaba, lakini alipambana na kuendelea na mchezo huo. 

Kipa huyo wa zamani wa Azam alicheza penalti mbili na Kariobangi Sharks kugongesha mtambaa wa panya penalti moja hivyo kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali kwa jumla ya mikwaju 3-2.

Meneja wa Simba, Richard Robert alisema daktari wa Simba, Yassin Gembe anaendelea na jitihada kuhakikisha kipa huyo anacheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Kakamega Homeboys. 

"Tunapambana na kuona anaweza kucheza mechi ijayo. Kuna daktari mwingine tumepanga kuzungumza naye ili asaidie uponaji wake wa haraka," alisema Robert.

No comments

Powered by Blogger.