Full-Width Version (true/false)


Mara paap! Simba hiyoo fainali na Singida United

 


Mashindano ya SportPesa hatua ya nusu fainali yataendelea leo Alhamisi ambapo timu za Tanzania, Simba na Singida United zitakuwa kibaruani nchini Kenya. 

Simba watakuwa na kazi moja kuhakisha wanaibuka na ushindi kwenye mechi ambayo wanakutana na wababe waliwatoa watani zao Yanga kwenye hatua ya awali. Mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Gor Mahia dhidi ya Singida United na utapigwa saa 7:00 mchana. 

Mchezo mwingine utawakutanisha wababe Kakamega Homeboys dhidi ya Simba mechi itakayochezwa saa 9:15 alasiri. 

Iwapo timu za Tanzania zitaibuka na ushindi, basi zitakuwa zimejiwekea uhakika kulileta kombe hilo nchini na timu mojawapo kwenda kucheza na Everton hapo baadaye.

No comments

Powered by Blogger.