Full-Width Version (true/false)


Maria na Consolata walijichagulia sehemu ya kuzikwa

 


Mkuu Shirika la Maria Consolata, Jane Nugi amesema kuwa mapacha Maria na Consolata watazikwa kwenye makaburi ya Tosamaganga kama walivyoomba wenyewe wakati wakiwa hai. 

Akizungumzia mazishi hayo jana Jumatatu, Juni 4, Jane amesema uamuzi huo umefikiwa kutokana na matakwa ya pacha hao ambao katika uhai wao walichagua kuzikwa kwenye eneo wanalozikwa viongozi wa madhehebu ya Katoliki na kwamba msiba wao upo kwenye nyumba ya shirika hilo Kihesa, Iringa kwa kuwa ndio nyumbani kwao. 

“Wakati wakiumwa walisema wangetamani kuhifadhiwa tunakohifadhiwa sisi hivyo watazikwa kwenye makaburi ya Tosamaganga,” amesema. 

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema kuwa pacha hao wanaandaliwa jeneza moja lenye mfumo wa watu wawili, misalaba miwili na kwamba watazikwa katika kaburi moja.

Kuhusu ratiba, Kasesela amesema wataagwa kesho Jumatano, Juni 6 katika viwanja vya Rucu ambako pia kutakuwa na ibada maalumu itakayoanza saa nne ikisimamiwa na maaskofu, Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo la Iringa na Alfred Maluma wa Jimbo Katoliki Njombe.

Makamu Mkuu wa Rucu, Pius Mgeni amesema, “Tumeshaanza maandalizi ya ujenzi wa jukwaa kwa ajili ya kuwaaga.” 

Mlezi wa wanafunzi wa Rucu, Martha Magembe amesema walilazimika kuunda zamu za kulala na kushinda hospitali na pacha hao baada ya walezi waliokuwa nao Muhimbili kutakiwa kupumzika

No comments

Powered by Blogger.