Full-Width Version (true/false)


Masaa saba ya upasuaji,Lissu abaini jipya
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru watanzania wote kiujumla kwa kuweza kumuombea na kutoka salama katika chumba cha upasuaji jambo ambalo amedai limempa matumaini makubwa ya kupona kabisa. 

Lissu ametoa neno hilo la shukrani asubuhi ya leo ikiwa imepita siku moja tokea alipomaliza kufanyiwa upasuaji huo ambao unakuwa wa 20 kufanyiwa mpaka hivi sasa ili kuweza kumsaidia kupona kabisa na kurejea katika harakati zake alizokuwa azifanyazo hapo awali.

"Hello wapendwa wangu nawasalimu wote kwa upendo mkubwa ile mbio ya marathon ya jana iliisha salama baada ya masaa saba. Sasa nimeingia kwenye hatua uponyaji, Mungu ni mwema amewawezesheni kuendelea kunipigania. Bila shaka ataniwezesha, kwa kupitia kwenu, kumalizia sehemu hii iliyobaki. Mungu awabariki sana na awaongezee mlikopungukiwa", amesema Lissu.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa na watu wasiojulikana tangu Septemba 7,2017 akiwa mkoani Dodoma, na kisha kupelekwa nchini Nairobi kwa matibabu na baada ya miezi 3 alipelekwa nchini Ubelgiji kwa hatua nyingine ya matibabu.

No comments

Powered by Blogger.