Full-Width Version (true/false)


Mashabiki Simba wachangamkia tuzo za MO Dewji

 


Mashabiki na wanachama wa Simba wameonyesha muitikio mkubwa katika kutafuta washindi wa tuzo maalum zilizoanzishwa na Mwekezaji na Mwanachama wa klabu hiyo Mohammed Dewji zijulikanazo kama 'MO Simba Awards 2018' Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia tuzo hizo, Mulamu Nghambi alisema upigaji kura limepokelewa kwa muitikio chanya na mashabiki na wanachama wao kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Nghambi alisema hakuna kigezo maalum kilichowekwa katika kuteua washindi mbalimbali wa tuzo hizo na badala yake mashabiki na wanachama wanapiga kwa utashi wao. 

Nghambi alisema Dewji ameamua kuanzisha tuzo hilo kwa lengo la kutambua mchango wa watu mbalimbali waliochangia mafanikio ya klabu hiyo.

No comments

Powered by Blogger.