Full-Width Version (true/false)


Mashabiki wa Yanga wabaki Kenya kwa ajili ya kuizomea Simba
 
Baada ya Yanga kung’olewa katika mechi yao ya kwanza ya michuano ya Kombe la SportsPesa Super Cup, mashabiki wake waliamua kubaki mjini hapa, kushuhudia mechi kati ya Simba dhidi ya Kariobang Sharks.
 

Mashabiki hao wa Yanga ambao jana walishuhudia dakika 90, Yanga iking’olewa kwa kufungwa na Kakamega Homeboys, leo waligeuka mwiba kwa Simba.
 

Mashabiki hao muda mwingi walikuwa wakiwazomea wachezaji wa Simba na kuwashangilia Sharks.
 

Kipindi cha kwanza, Sharks waliwazidia Simba na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga, kipa Aishi Manula akiwa shujaa.
 

Katika kipindi cha pili, Simba walibadilika lakini bado hawakuwa na madhara makubwa kwa Wakenya hao.
 

Wakati wa penalti, mashabiki hao walikuwa wakipiga kelele kutaka Manula aondoe taulo langoni mwake.

No comments

Powered by Blogger.