Full-Width Version (true/false)


Mbao FC yamchukua kocha wa Simba

 

Kikosi cha Wafanyabiashara wa Mbao, Mbao FC ya Mwanza, kimemnasa Kocha Amri Said na ndiye atakayeinoa timu hiyo kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu Bara. 

Amri Said ametua Mbao na kusaini mkataba wa miaka miwili baada ya kumalizana na Lipuli FC ya Iringa aliyoifundisha msimu uliopita akisaidiana na 'swahiba' wake Seleman Matola. Mchezaji huyo na kocha wa zamani wa Simba, amechukua mikoba ya kuifundisha Mbao iliyoachwa na kocha Mrundi Ettiene Ndayiragije ambaye ametimkia KMC. 

Mbao imemaliza ligi ikiwa kwenye nafasi ya 13 kwenye ligi yenye timu 16 na kunusurika kidogo kushuka daraja.

No comments

Powered by Blogger.