Millard Ayo azushiwa kifo,mwenyewe aibuka kukanusha “mimi ni mzima kabisa”
Leo June 07,2018 katika mitandao ya
kijamii ilisambaa taarifa ambayo si mzuri ikidai kuwa mtangazaji maarufu nchini ,Millard Ayo amefariki
Dunia.
Kufuatia taarifa hizo “feki” ambazo
zilizua hofu na mshituko mkubwa, Millard Ayo amejitokeza na kueleza kwamba yeye
ni mzima wa afya njema kabisa.
Ayo ameyasema hayo kwenye video fupi
aliyejirekodi akiwa anasema maneno yafuatayo.
“Asanteni sana watu wangu wote ambao mmeniandikia
,mmenipigia simu kuhusiana na taarifa ambazo zinasambazwa juu yangu. Mimi ni
mzima wa afya kabisa ,napenda niwafahamishe mimi ni mzima wa afya kabisa. Lakini
nawashukuru sana wote ambao mmenipigia simu, mmeniandikia dm ,mmeniandikia sm
kuonesha upendo wa hali ya juu kutaka kujua hali yngu ya kiafya,mimi ni mzima
wa afya kabisa na nawatakia jioni njema”.amesema Millard Ayo.
msikilize haapa chini
No comments