Full-Width Version (true/false)


MINZIRO AFUNGUKA KWA KUELEZA HAYA BAADA YA KUONDOLEWA KMC ALIYOIPANDISHA DARAJA


Aliyekuwa Kocha wa KMC FC kutoka Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Fredrick Minziro, amefunguka kwa kueleza kuwa hajaona tatizo kuondolewa katika nafasi hiyo iliyochukuliwa na Mrundi, Etienne Ndayiragije.


Minziro ambaye aliipandisha daraja KMC mpaka Ligi Kuu Bara ameondolewa kwenye kikosi hicho baada ya Kocha Ndayiragije aliyewahi kuifundisha Mbao FC akichukua mikoba yake.


Kutokana na kuondoshwa kwake Minziro, ameeleza kuwa yeye amelipokea kawaida tu kutokana nafasi hiyo ina taaluma yake japo akiahidi kuelez mengi Jumanne ya wiki ijayo atakapoitisha kikao na Waandishi wa Habari.


Leo klabu hiyo imemtangaza rasmi Ndayiragije kuwa Kocha Mkuu wa KMC tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.


Ikumbukwe tu kuwa Minziro aliwahi kuipandisha pia Singida United kucheza Ligi Kuu msimu wa 2016/17 lakini akaondolewa na Mholanzi, Hans van der Pluijm akachukua nafasi yake akitokea Yanga.

No comments

Powered by Blogger.