Full-Width Version (true/false)


Misri yashindwa kumfariji mohamed Salah dhidi ya Colombia


Timu ya taifa ya Misri imeshindwa kutamba mbele ya Colombia baada ya kwenda suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa kirafiki.


Misiri imeshindwa kumfariji nyota wake, Mohamed Salah ambaye anauguza majeraha baada ya kuumia katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid Mei 26 2018.


Mechi hiyo imeshindwa kutoa mbabe ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya Kombe la Dunia huko Russia.


Inaelezwa kuwa Salah atakosa mechi ya kwanza wakati Misri itakapofungua pazia la michuano hiyo dhidi ya Uruguay Juni 15 2018.

No comments

Powered by Blogger.