Full-Width Version (true/false)


Mke na Mume wafikishwa mahakamani kwa biashara ya madawa ya kulevya

 


Mfanyabishara Ayoub Kiboko na anayedaiwa kuwa mkewe, Pilly Kiboko wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za Uhujumu Uchumi ikiwamo kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin. 

Wanafamilia hao walisomewa mashtaka yao Ijumaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo. 

Wakili wa Serikali Mwandamizi Patrick Mwita alidai kuwa Mei 23, mwaka huu, maeneo ya Tegeta Nyuki Masaiti, Dar es Salaam washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo. Alidai washtakiwa walikutwa wakisafirisha gramu 251.25 za dawa za kulevya aina ya heroin. 

Hata hivyo, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika na kuhamishiwa Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi. Hakimu Simba alisema kesi hiyo itatajwa Juni 15 na washtakiwa wapelekwe mahabusu.

No comments

Powered by Blogger.