Full-Width Version (true/false)


Mkemi ameamua kubwaga manyanga Yanga


 
 
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi ameamua kubwaga manyanga.


Mkemi ametangaza kuachia ngazi katika nafasi yake hiyo jana kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram, mara tu baada ya Yanga kufungwa mabao 3-1 na timu ya Kakamega Homeboyz.
 
"Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi
Kwa Hakika Tumepata Aibu
Kubwa
Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili
Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza
Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikikwaza.
Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club "YANGA " kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.
Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu
SALUM MKEMI
NIMENG'ATUKA"

Kakamega Homeboyz wameing’oa Yanga kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na leo  itaondoka kurejea nyumbani Tanzania.

Kitendo hicho kinaonekana kumkwaza Mkemi ambaye amesema anatoa nafasi kwa mawazo mapya.

Juhudi za kumpata Mkemi hazijafanikiwa kwa kuwa simu yake imekuwa ikiita muda mrefu bila kupokelewa.

Rafiki mmoja wa Mkemi amesema kwamba Mkemi alikerwa sana na kipigo hicho lakini wiki moja kabla amekuwa akizungumzia suala la kujiuzulu ingawa hakuwa amechukua hatua rasmi.

Juhudi nyingine zilifanyika ni kuupata uongozi wa Yanga mjini hapa na hasa Hussein Nyika ambaye amekuwa akifanya kazi kwa karibu na Mkemi, lakini naye simu yake haikupokelewa.

Hivi karibuni, kulikuwa na taarifa za kujiuzulu kwa Mkemi, lakini baadae mwenyewe aalijitokeza kulalamika

No comments

Powered by Blogger.