Full-Width Version (true/false)


Mlemavu aliyepasua masomo asaidiwa
Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Lufulu wilayani Kilombero ambaye ni mlemavu, Ezra Mwambasi, licha ya kukabiliwa na changamoto za kimaisha lakini anafanya vyema kitaaluma. Ezra (12), anayeishi katika mazingira yasiyo rafiki ameshika nafasi ya nane katika matokeo ya wilaya kwenye mtihani wa taifa wa darasa la nne mwaka 2017. 

Akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa baiskeli ya magurudumu matatu, mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunyo alisema wenye ulemavu wana haki ya kupata huduma za kijamii ikiwamo elimu. 

Ihunyo aliwataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu kuhakikisha wanawapeleka shule na kuacha tabia ya kuwafungia nyumbani. 

Naye Ezra alisema kwamba baiskeli hiyo itamsaidia kwa usafiri na kumwezesha kufika shuleni kwa wakati. Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Fadhil Mkhoi alisema mwanafunzi huyo anaonyesha juhudi darasani kwa kufanya vyema kitaaluma tangu shule ya awali

No comments

Powered by Blogger.