Modric ampeleka Neymar Real Madrid
Kiungo Luka
Modric
amemwambia
Neymar anasubiri
kwa hamu kubwa
huko Real Madrid
wakati wawili hao
walipokutana kwenye mechi ya kirafiki baina ya timu zao za taifa
Brazil na Croatia juzi Jumapili uwanjani Anfield jijini Liverpool,
England.
Mwanasoka huyo ghali duniani, Neymar kwa muda mrefu
amekuwa akiripotiwa ana mpango wa kuihama timu yake ya Paris
Saint-Germain na kutimkia Real Madrid na Mbrazili huyo
haonekani kupuuzia hicho kinachozungumzwa.
Hiyo juzi, Neymar alicheza kwa mara ya kwanza baad ya kuwa nje
kwa siku 99 na haraka sana akafunga bao kuisaidia Brazili
kuichapa Croatia 2-0.
Baada ya mechi, Neymar na Modric walikutana kwenye kolido za
Uwanja wa Anfield na kila mmoja akiwa anasaini jezi ya
mwenzake, kiungo wa Madrid na Croatia, Luka alimwambia
Neymar: "Tunakusubiri."
PSG ilivunja rekodi ya dunia wakati ilipolipa Pauni 198 milioni
kunasa huduma ya Neymar kwenye majira ya kiangazi mwaka jana
akitokea Barcelona na sasa Madrid inataka kumrudisha kwenye La
Liga msimu ujao.
Mpango wa Madrid ni kufanya usajili wa mastaa wa maana licha
ya kupigwa na butwaa kufuatia aliyekuwa kocha wake Zinedine
Zidane kuachana na timu hiyo.
No comments