Full-Width Version (true/false)


Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa wapata ajali

 


Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James umepata ajali katika eneo la Kisesa wilayani Meatu mkoani Simiyu. 

Akizungumza na MCL Digital leo Jumapili Juni 10, 2018 kwa njia ya simu, James amesema baadhi ya watu wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kukimbizwa hospitali huku akitaka atafutwe Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kwa taarifa zaidi. 

Kamanda wa Polisi mkoani Simiyu, Boniventure Mushongi akizungumza na MCL Digital amesema ni kweli ajali hiyo imetokea lakini anasubiri kupatiwa ripoti kamili. 

“Ni kweli taarifa za awali zinasema hivyo, inasemekana kuna basi limeligonga gari lao kwa nyuma,” amesema Mushongi na kuahidi kutoa taarifa kamili baadaye. Akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter ya umoja huo inaeleza kuwa ajali hiyo imetokea muda mfupi baada ya msafara huo kuingia Meatu, ukitokea wilaya ya Itilima. 

“Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James umepata ajali eneo la Kisesa wilayani Meatu,” unaeleza ujumbe huo. Unaeleza kuwa mwenyekiti huyo wa UVCCM na maofisa aliofuata nao hawajajeruhiwa.

No comments

Powered by Blogger.