Full-Width Version (true/false)


Mtoto wa Ngwair amtoa 'shipa' Dully Sykes


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya , Dully Sykes amefunguka na kudai amesikitishwa na swahiba wake marehemu Albert Mangwear kufariki bila ya kuacha mtoto hata mmoja ambaye angeweza kumsomea dua katika kumbukumbu ya siku ya kifo chake. 
Dully ametoa kauli hiyo leo Juni 11, 2018 wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo 'PB' kinachorushwa na East Africa Radio na kuwataka wasanii wenzake waungane ili watengeze mazingira ya kumsomea dua Mangwear kila ifikapo Mei 28 kwa kuwa hana mtoto wa kumfanyia hivyo na yeye binafsi hana uwezo wa kufanya jambo hilo pekee yake.

"Mimi nasikitika kwamba Albert Mangwear amefariki hajaacha hata mtoto maana najua ingemsaidia japokuwa asingepata heshima hiyo lakini heshima ya mtoto kuenda kumuekea ubani kanisani au kumsomea baba yake dua ni heshima kubwa sana katika siku yake ya kufariki", amesema Dully.

Pamoja na hayo, Dully ameendelea kwa kusema "kwasababu Mangwear hakuacha mtoto kwanini sasa sisi wasanii tusishirikiane kumsomea dua siku ambayo kifo chake kilitokea. Kiukweli mimi natamani nifanye hivyo ila tatizo sina uwezo kiukweli kabisa wa kuandaa kiu kikubwa kila mwaka".

Kwa upande mwingine, Dully amesema anazikumbuka harakati za marehemu Mangwear walizokuwa wakifanya pamoja enzi alipokuwa hai.

No comments

Powered by Blogger.