Full-Width Version (true/false)


Mtungi wa gesi wateketeza nyumba Dodoma
Moto mkubwa unaosemekana umesababishwa na kulipuka kwa jiko la nishati ya gesi umeteketeza nyumba moja yenye vyumba sita iliyopo katika mtaa wa hazina x jijini Dodoma na kuharibu mali za baadhi ya wapangaji waliokuwa wakiishi ndani ya nyumba hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya wapangaji wa nyumba hiyo Maimuna Hussein na Nickson Steven wamesema moto huo umetokea saa 3:40 asubuhi na kuteketeza baadhi ya mali zao.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoji mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi Regina Kaombwe, amesema baada ya kupata taarifa ya kuungua kwa nyumba hiyo waliwahi eneo la tukio na kisha ametoa wito kwa wakazi wa jiji hilo.

No comments

Powered by Blogger.