Full-Width Version (true/false)


Mwanamke amuuwa mwanae kwa maweJeshi la Polisi katika eneo la Murang’a kaunti ya Kangema nchini Kenya, linamshikilia mwanamke mmoja kwa tuhuma za kumpiga na mawe mtoto wake wa miaka mitatu na kupelekea kifo chake. 
Kwa mujibu wa gazeti Daily Nation, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Juni 11 2018 katika Kijiji cha Tuthu, mwanamke huyo pia alimshambulia mama yake kwa mawe ambapo alijeruhiwa na kusadikika kuwa mwanamke huyo huenda ana matatizo ya akili.

Mashahidi katika eneo hilo wamedai kuwa mwanamke huyo alianza kurusha mawe kwa watu waliopo katika eneo hilo na kisha badae waliona mwili wa mtoto ukiwa umelala chini ndipo waliamua kuita viongozi wa eneo hilo.

Akithibitisha tukio hilo kamanda wa Polisi katika eneo la Kangema, kamanda OCPD Ben Kipkoech amesema mtuhumiwa huyo atakabiliwa na kosa la mauji ingawa Jeshi la Polisi limepata taarifa za kuwa mwanamke huyo ana matatizo ya akili lakini watahitaji ripoti ya daktari kuthibitisha.

Mwanamke huyo atapandishwa kizimbani siku ya Jumanne kujibu tuhuma za mauji, na mwili wa mtoto huyo umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Murang’a.

No comments

Powered by Blogger.