Full-Width Version (true/false)


Mwanamke anapaswa ampe 'shikamoo' mwanaume
Msanii wa muziki wa dansi nchini, Pancho Mwamba amedai kwamba wanawake wanapaswa kuheshimu waume zao kama wanavyoheshimu baba zao na kutakiwa kuamkia kama ishara ya kuonesha upendo na heshima kwa mume. 

Pancho amesema hayo leo Juni 6, 2018 katika kipindi cha DADAZ kinachorushwa na EATV kila siku ya Jumatano saa 5:00 asubuhi mpaka 6:00 mchana, na kuongeza kuwa kitendo cha kumuamkia mwanaume sio jambo baya na ndio maana mwanamke akiolewa hubadirisha jina la ukoo na kuchukua la mume wake.

“Unajua kwanza mume wako ni baba yako, ukishaolewa jina la baba linapotea, kusema shikamoo mume wangu sio kwamba ni lazima bali ni hali ya mahaba na heshima mnawekeana kwenye mood nzuri tu, hiyo ipo ila sio lazima ni chachu” amesema Pancho.

Msanii huyo ameongeza kuwa, ndoa nyingi sasa zinashindwa kudumu kwasababu baadhi ya wanawake kupenda kuiga mahusiano katika filamu za nchi za magharibi na kuhamishia katika utamaduni wa maisha ya mtanzania.

Pancho ambaye yupo katika ndoa kwa miaka 16 amesema kuwa kama baba wa familia hawezi kuchanganya maisha yake ya usanii na kuleta ndani ya nyumba na kudai kuwa usanii wake unaishia akifika katika mlango wa nyumba yake.

No comments

Powered by Blogger.