Full-Width Version (true/false)


Mwashiuya azichonganisha KMC, Azam

 
Winga aliyemaliza mkataba wake Yanga, Geofrey Mwashiuya amesema, Azam FC na KMC zinamuhitaji kwenye vikosi vyao lakini ameiachia nafasi ya kwanza timu yake ya Jangwani. 

Mwashiuya ambaye kwa sasa yuko kwao Mbeya kwa mapumziko, lakini Yanga bado haijamwongezea mkataba mpya baada ya ule wa awali wa miaka mitatu kumalizika. 

"Niko nyumbani kwetu Mbeya kwa mapumziko lakini bado sijapewa mkataba mpya na Yanga naendelea kuwasikilizia kwanza,"alisema Mwashiuya aliyesajiliwa na Yanga akitokea Kimondo ya Mbeya. 

Alipoulizwa kama kuna timu nyingine zimepeleka maombi kwake, Mwashiuya amesema: "Zipo nyingi tu kama Azam na KMC lakini naangalia kwanza mpango wa timu ya Yanga." Amesema, anaweza kufanya maamuzi mengine endapo Yanga aliowapa nafasi ya kwanza wataamua kutomwongezea mkataba mpya.

No comments

Powered by Blogger.