Full-Width Version (true/false)


Mwili wa Mwanajeshi aliyeuawa Afrika ya Kati waagwa kambini Lugalo


 

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga la Taifa, Dkt Hussein Mwinyi jana  ameongoza zoezi la kuaga miwili wa askari wa jeshi la ulinzi wa wananchi wa Tanzania Nsevilwe Nzowa aliyeuawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

 Akizungumza baada ya zoezi la kuaga mwili Waziri Mwinyi amesema wamepokea tukio hilo kwa majonzi na kuwasihi mashujaa kutokata tamaa katika kutimiza majukumu yao katika kulinda na kutetea amani. 

Aidha Waziri Mwinyi amesema kuwa serikal tayari imeunda tume ili kuchukua tahadhari dhidi ya mashujaa ambao wapo katika nchini mbalimbali katika kulinda amani. 

Mwili wa Marehemu Private Nsenvilwe Nzowa alifariki baada ya kupigwa risasi na kikundi kinachosadikiwa kuwa ni siri tarehe tatu siku ya jumapili umesafirishwa jana kuelekea kijiji cha Igamba wilayani Mbozi mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika kesho jumapili.

No comments

Powered by Blogger.