Full-Width Version (true/false)


Manula: Gor Mahia anakufa ndani ya dakika 90
Nakuru. Kipa wa Simba, Aishi Manula anaamini kuwa pambano lao la fainali dhidi ya Gor Mahia litaisha kwenye dakika 90 bila kushuhudia mikwaju ya penalti kama ilivyotokea kwenye mechi mbili za awali. 

Manula alisema kikosi chao kipo vizuri kuelekea kwenye mchezo wa fainali na wachezaji wamejipanga kumaliza mchezo ndani ya dakika 90. 

Simba ilishuhudia mechi zake mbili za awali zikiamuliwa kwa mikwaju ya penalti kitendo ambacho kimewaweka roho juu mashabiki wa timu hiyo jambo ambalo Manula hataki litokee kwenye fainali. 

"Namshukuru Mungu kwa kucheza vizuri katika hatua za awali mpaka sasa, lakini naamini kuwa mechi ya fainali haitafika kwenye penalti, tutaimaliza mapema," alisema Manula.

No comments

Powered by Blogger.