Full-Width Version (true/false)


Ndalichako amuomba Waziri Mwalimu kuwasaidia pacha wengine walioungana

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako amemuomba Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuwasaidia watoto wengine pacha walioungana kama walivyokuwa Maria na Consolata. 

Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo Juni 6 katika mazishi ya pacha walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti, yaliyofanyika, Iringa. 

Amesema kila mtoto amezaliwa kwa namna yake hivyo kuwasaidia kutawafanya wakue vizuri kama ilivyo kwa Maria na Consolata. 

“Ni wakati kwa jamii kutokubali kuwaficha watu wenye ulemavu kwa kuwa wakipewa maarifa wanaweza kufanya mambo makubwa,” amesema Pacha wengine wenye umri wa miezi mitano, wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili walikohamishiwa wakitokea, Kituo cha Afya cha Misenyi, Kagera.

No comments

Powered by Blogger.