Ndalichako: Maria na Consolata ‘mashujaa wa taifa’
"Ni mashujaa wa taifa letu" hiki ndicho alichosema Waziri wa
Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako baada ya kutoa
heshima za mwisho kwa miili ya pacha walioungana, Maria na
Consolata Mwakikuti.
Akizungumza leo Juni 5 mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa
miili ya pacha hao, Profesa Ndalichako amesema mashujaa hao
wameliacha taifa katika simanzi nzito.
"Mara ya mwisho niliwaona pale Mwaisela wakiwa wodi ya wagonjwa
mahututi, inaniumiza mno lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe,"
amesema.
Amesema wizara hiyo imepoteza watu muhimu waliokuwa wakipigania
elimu bila kujali ulemavu na namna walivyo.
No comments