Ndugu wa marehemu Sam wa Ukweli wamlaani aliyesema kafariki kwa UKIMWI, wenyewe waeleza kilichomuua

Ndugu wa marehemu Sam wa Ukweli wamemjia juu producer wa muziki
ambaye alikuwa wa kwanza usiku wa jana kutoa taarifa za kifo cha ndugu
yao kinyume na taratibu huku akitangaza kuwa marehemu alikuwa anaugua
ugonjwa wa UKIMWI wa kurogwa.
Mdogo na mjomba wa marehemu Sam wa Ukweli wamesema kuwa marehemu
amekufa kwa malaria na UTI na magonjwa hayo yameanza kumsumbua tangu
ijumaa ya wiki iliyopita baada ya kuwasili kutoka Singida alikoenda
kwenye show.
kesho mwili wa marehemu
unatarajiwa kusafirishwa kwenda Bagamoyo kwa ajili ya mazishi.
No comments