Full-Width Version (true/false)


Nigeria yaaongoza kuwa naa jezi mzuri za kombe la gunia,ikifuatiwa na Ufaransa


Mashabiki mbalimbali wa soka duniani, wamezichagua jezi za Nigeria kuwa namba moja kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia.

Mashabiki hao kupitia mitandao mbalimbali ukiwemo ule wa Gazeti la Marca la Hispania, wametoa namba moja kwa jezi ya Nigeria kwamba inavutia sana.

Jezi inayofuatia kwa kuvutia ni lie ya Ufaransa ambayo mashabiki wameipa namba mvili na namba tatu imekwenda kwa Croatia.

Ujerumani imeshika nafasi ya nne, tano imekwenda kwa Iceland na ’namba sita ni Mexico.
Hivi karibuni, jezi za Nigeria zilizotengenezwa na Nike, zilinunuliwa kama njugu na kuzua gumzo kubwa.

No comments

Powered by Blogger.