Full-Width Version (true/false)


Nikipata wimbo wa kufanya na msanii wa WCB nitafanya lakini… – Abdul Kiba
Msanii wa muziki, Abdul Kiba amedai kama akipata ngoma ambayo ataona anahitajika msanii kutoka WCB ashiriki anatafuta na kufanya naye kazi kwa kuwa hakuna tatizo lolote kati yao.

Muimbaji huyo amesema mpaka sasa bado hajapata kazi ambayo anaona kuna haja ya kumtafuta msanii yeyote wa kundi hilo lilipo chini rais wa wake, Diamond Platnumz.

“Kufanya kolabo na msanii yeyote kutoka WCB inategemeana na muziki gani ambao nimeimba, naamini kila muziki una sura ambayo inaonyesha ni nani unaweza kuimba naye, ikitokea kuna muziki ambao naona kuna haja ya msanii kutoka WCB nitafanya naye na kama sina tutabaki hivi hivi WCB na Team Kiba,” Abdukiba aliimbia EFM.

Mashabiki wa muziki wanatamani siku moja kushuhudia kolabo ya msanii kutoka WCB na msanii kutoka Team Kiba.

Meneja wa Diamond, Mkubwa Fella akiahidi siku moja atahakikisha wawili hao wanafanya kolabo huku akitoa nafasi kwa upande wa Alikiba kama wataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

No comments

Powered by Blogger.