Full-Width Version (true/false)


“Nimezungukwa na masnitch”- TIDMsanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Khaleed Mohamed ‘TID’, amefunguka kuwa tangu alipofariki Albert Mangwea hajawahi pata rafiki wa kweli kwa kipindi chote cha miaka mitano. 

TID ameiambia eNewz ya East Africa Televisheni kuwa wasanii wengi wanafanya kazi kwa chuki na majungu hali inayopelekea kushindwa kusaidiana kufikisha sanaa kimataifa jambo ambalo linasababisha migogoro baina yao.

“Wasanii wengi wamebaki kusema mabaya ya wenzao na si kuwa msaada, na wengine walifurahia kifo cha rafiki yangu ndio maana nasema wamebaki ‘masnitch’ kibao”, amesema TID

Hii imejiri baadaya kumbukumbu ya miaka mitano tangu kufariki kwa mfalme huyo wa ‘freestyle’ Albert Mangwea ambaye alifariki tarehe 28 mwezi mei mwaka 2013. Mtazame hapo chini TID amefunguka zaidi

No comments

Powered by Blogger.